[go: up one dir, main page]

Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 2 Oktoba 2025

Utangulizi wa Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs)

EIPs ni nini?

Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs)opens in a new tab ni viwango vinavyobainisha vipengele vipya vinavyowezekana au michakato ya Ethereum. EIPs zina maelezo ya kiufundi ya mabadiliko yanayopendekezwa na hufanya kama "chanzo cha ukweli" kwa jumuiya. Visasisho vya mtandao na viwango vya matumizi ya Ethereum vinajadiliwa na kuendelezwa kupitia mchakato wa EIP.

Mtu yeyote ndani ya jumuiya ya Ethereum ana uwezo wa kuunda EIP. Miongozo ya kuandika EIP imejumuishwa katika EIP-1opens in a new tab. Pendekezo la uendelezaji wa Ethereum inapaswa kwanza kutoa maelezo ya kiufundi kwa ufupi pamoja na kiasi kidogo cha sababu ya msingi. Mwandishi wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum ana jukumu la kufanikisha makubaliano ndani ya jumuiya na kuandika maoni mbadala. Kutokana na kizuizi kubwa kiufundi cha kuwasilisha pendekezo la uendeleshaji wa Ethereum iliyoandikwa vizuri, waandishi wengi wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum kwa kawaida ni waendelezaji wa maombi rasmi au watengenezaji wa itifaki.

Kwa nini EIPs ni muhimu?

EIPs huchukua jukumu kuu katika mabadiliko yanavyotokea na kurekodiwa kwenye Ethereum. Ni njia ya watu kupendekeza, kujadili, na kupitisha mabadiliko. Kuna aina tofauti za EIPopens in a new tab, ikiwa ni pamoja na EIP za msingi za mabadiliko ya itifaki ya kiwango cha chini ambayo huathiri makubaliano na kuhitaji uboreshaji wa mtandao kama vile EIP-1559opens in a new tab, na ERC za viwango vya programu kama vile EIP-20opens in a new tab na EIP-721opens in a new tab.

Kila uboreshaji wa mtandao unajumuisha seti ya EIP ambazo zinahitaji kutekelezwa na kila mteja wa Ethereum kwenye mtandao. Hii inamaanisha kuwa ili ubaki kwenye makubaliano na wateja wengine kwenye mtandao mkuu wa Ethereum, watengenezaji wa wateja wanahitaji kuhakikisha kuwa wote wameutekeleza pendekezo la uendelezaji wa Ethereum zinazohitajika.

Pamaoja na kutoa maelezo ya kiufundi kwa ajili ya mabadiliko, EIPs ni kitengo amabacho usimamizi wake hufanyika ndani ya Ethereum: mtu yeyote yuko huru kutoa pendekezo, na kisha wadau mbalimbali katika jamii watajadiliana ili kubaini kama inafaa kupitishwa kama kiwango au kujumuishwa katika uboreshaji wa mtandao. Kwa kuwa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum zisizo za msingi hazihitzjiki kuzuiliwa maombi rasmi wowote ( mfano, inawezekana kuunda tokeni inayoweza kubadilishwa ambayo haitekelezi pendekezo la uendelezaji wa Ethereum-20) lakini pendekezo la uendelezaji wa Ethereum za msingi lazima zikubalike kwa wingi (kwa kuwa vituo zote lazima zipate masasisho ili kubaki sehemu ya wavu mmoja) Pendekezo la uendelezaji wa Ethereum za msingi zinahitaji makubaliano pana zaidi ndani ya jumuiya kuliko pendekezo la uendelezaji wa Ethereum zisizo za msingi.

Historia ya EIP

Hazina ya GitHub ya Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs)opens in a new tab iliundwa mnamo Oktoba 2015. Mchakato wa EIP unatokana na mchakato wa Mapendekezo ya Kuboresha Bitcoin (BIPs)opens in a new tab, ambao nao unatokana na mchakato wa Mapendekezo ya Kuboresha Python (PEPs)opens in a new tab.

Wahariri wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum wanapewa jukumu la kuchunguza pendekezo la uendelezaji wa Ethereum kwa usahihi wa kiufundi, masuala ya muundo, na kusahihisha tahajia, sarufi, na mtindo wa maandiko ya programu. Martin Becze, Vitalik Buterin, Gavin Wood na wengine wachache ndio wahariri waanzilishi wa EIP kutoka mwaka 2015 kwenda mwishoni mwa mwaka 2016.

Wahariri wa sasa wa EIP ni

  • Alex Beregszaszi (@axic)
  • Gavin John (@Pandapip1)
  • Greg Colvin (@gcolvin)
  • Matt Garnett (@lightclient)
  • Sam Wilson (@SamWilsn)

Wahariri wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum wa heshima ni.

  • Casey Detrio (@cdetrio)
  • Hudson Jameson (@Souptacular)
  • Martin Becze (@wanderer)
  • Micah Zoltu (@MicahZoltu)
  • Nick Johnson (@arachnid)
  • Nick Savers (@nicksavers)
  • Vitalik Buterin (@vbuterin)

Ikiwa ungependa kuwa mhariri wa EIP, tafadhali angalia EIP-5069opens in a new tab.

Wahariri wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum wanaamua ni lini pendekezo liko tayari kuwa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum, na kuwasaidia waandishi wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum kusogeza pendekezo lao mbele. Ethereum Cat Herdersopens in a new tab husaidia kuandaa mikutano kati ya wahariri wa EIP na jumuiya (tazama EIPIPopens in a new tab).

Mchakato kamili wa usanifishaji pamoja na chati umeelezwa katika EIP-1opens in a new tab

Jifunze zaidi

Ikiwa ungependa kusoma zaidi kuhusu EIP, angalia tovuti ya EIPopens in a new tab na EIP-1opens in a new tab. Hapa kuna viungo vya muhimu.:

Miradi ya elimu ya jumuiya

  • PEEPanEIPopens in a new tabPEEPanEIP ni mfululizo wa video za elimu unaojadili Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs) na sifa muhimu za maboresho yajayo.
  • EIPs.wtfopens in a new tabEIPs.wtf hutoa maelezo ya ziada kwa ajili ya Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs), ikiwa ni pamoja na hali zake, maelezo ya utekelezaji, pull requests zinazohusiana, na maoni ya jumuiya.
  • EIP.Funopens in a new tabEIP.Fun hutoa habari za hivi punde kuhusu Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs), masasisho kuhusu mikutano ya EIP, na zaidi.
  • EIPs Insightopens in a new tabEIPs Insight ni uwakilishi wa hali ya mchakato wa Mapendekezo ya Kuboresha Ethereum (EIPs) na takwimu kulingana na taarifa zilizokusanywa kutoka vyanzo tofauti.

Shiriki

Kila mtu anaweza kuunda pendekezo la uendelezaji wa Ethereum. Kabla ya kuwasilisha pendekezo, ni lazima mtu asome EIP-1opens in a new tab ambayo inaelezea mchakato wa EIP na jinsi ya kuandika EIP, na kutafuta maoni kwenye Ethereum Magiciansopens in a new tab, ambapo mapendekezo hujadiliwa kwanza na jumuiya kabla ya rasimu kuwasilishwa.

Marejeleo

Maudhui ya ukurasa yaliyotolewa kwa sehemu kutoka Utawala wa Maendeleo ya Itifaki ya Ethereum na Uratibu wa Uboreshaji wa Mtandaoopens in a new tab ulioandikwa na Hudson Jameson

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 2 Oktoba 2025

Je! makala haya yamekusaidia?