[go: up one dir, main page]

Ruka kwenda kwenye maudhui makuu

Ukurasa ulisasishwa mwisho: 15 Februari 2026

Utangulizi wa utawala wa Ethereum

Kama hakuna mmoja anayemiliki Ethereum, maamuzi yana tengenezwaje kuhusu mabadiliko ya zamani na mbeleni ya Ethereum? Utawala wa Ethereum unahusu mchakato unaoruhusu maamuzi kama hayo kufanywa.

Ni nini maana ya uongozi.?

Uongozi ni mfumo uliopo inaruhusu maamuzi kufanywa. Katika muundo wa kawaida ya shirika, timu ya utendaji au bodi ya wakurugenzi inaweza kuwa na uamuzi wa mwisho katika kufanya maamuzi. Au labda wamiliki wa hisa wanapiga kura juu ya mapendekezo ili kutekeleza mabadiliko. Katika mfumo wa kisiasa, maafisa waliochaguliwa wanaweza kutunga sheria zinazojaribu kuwakilisha matakwa ya wapiga kura wao.

Utawala uliogatuliwa

Hakuna mtu mmoja anayemiliki au kudhibiti itifaki ya Ethereum, lakini bado maamuzi yanahitaji kufanywa kuhusu kutekeleza mabadiliko ili kuhakikisha uhai mrefu na ustawi wa wavu. Ukosefu huu wa umiliki unafanya uongozi wa kawaida wa kiasasi usiendane na suluhisho.

Utawala wa Ethereum

Uongozi wa Ethereum ni utaratibu ambao kupitia kwake mabadiliko ya itifaki hufanywa. Ni muhimu kuonyesha kwamba utaratibu huu hauna uhusiano na jinsi watu na maombi rasmi zinazotumia itifaki - Ethereum haina ruhusa. Kila mtu kutoka sehemu yoyote duniani anaweza kushiriki katika shughuli zinazofanyika kwenye mnyororo wa vizuizi. Hakuna kanuni maalum za nani anaweza au hawezi kuunda maombi rasmi au kufanya muamala. Hata hivyo, kuna utaratibu wa kupendekeza mabadiliko kwenye itifaki kuu, ambayo maombi rasmi zisizo za kudhibitiwa kati inaendeshwa juu yake. Kwa kuwa watu wengi hutegemea uthabiti wa Ethereum, kuna kiwango cha juu sana cha ushirikiano inachohitajika kwa mabadiliko makuu, ikiwemo taratibu za kijamii na kiteknolojia, kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote ya Ethereum ni salama na yanayoungwa mkono sana na jamii.

Utawala wa Onchain dhidi ya offchain

Teknolojia ya mnyororo wa vizuizi unaruhusu uwezekano mpya wa uongozi, unaojulikana kama uongozi wa mnyororo wa vizuizi vya ndani. Uongozi wa mnyororo wa vizuizi vya ndani ni pale ambapo mabadiliko yaliyopendekezwa ya itifaki yameamuliwa kupitia kura ya washiriki wenye maslahi, kawaida kwa wamiliki wa tokeni ya uongozi, na upigaji kura unafanyika kwenye mnyororo wa vizuizi. Katika baadhi ya mifumo ya uongozi wa mnyororo wa vizuizi vya ndani, mabadiliko iliyopendekezwa tayari yameandikwa kwenye msimbo na hufanyiwa utekelezaji moja kwa moja ikiwa washiriki wenye maslahi watakubali mabadiliko hayo kwa kuweka sahihi muamala.

Njia kinyume chake, uongozi wa mnyororo wa vizuizi vya nje, ni pale ambapo maamuzi yoyote kuhusu mabadiliko ya itifaki hufanywa kupitia utaratibu usio rasmi wa majadiliano ya kijamii, ambayo, ikiwa itakubaliwa, inatekelezwa katika msimbo ili kutekelezwa.

Utawala wa Ethereum hufanyika offchain kukiwa na washikadau mbalimbali wanaohusika katika mchakato huo.

Ingawa katika kiwango cha itifaki utawala wa Ethereum ni offchain, kesi nyingi za utumiaji zilizojengwa juu ya Ethereum, kama vile DAOs, hutumia utawala wa onchain.

Zaidi kuhusu DAOs

Ni nani washiriki.?

Kuna washikadau mbalimbali katika jamii ya Ethereum, kila mmoja akichukua jukumu katika mchakato wa utawala. Kuanza na washiriki wenye maslahi wali mbali zaidi na itifaki na kisha kuzingatia kwa karibu, tunayo.:

  • Wamiliki wa Ether: watu hawa wanamiliki kiasi chochote cha ETH. Zaidi kuhusu ETH.
  • Watumiaji wa Programu: watu hawa huingiliana na programu kwenye blockchain ya Ethereum.
  • Wasanidi wa Programu/Zana: watu hawa huandika programu zinazoendeshwa kwenye blockchain ya Ethereum (k.m., DeFi, NFTs, n.k.) au huunda zana za kuingiliana na Ethereum (k.m., mikoba, seti za majaribio, n.k.). Zaidi kuhusu mfumo mtawanyo wa kimamlaka.
  • Waendeshaji wa Nodi: watu hawa huendesha nodi zinazoeneza vizuizi na miamala, na kukataa muamala au kizuizi chochote batili wanachokipata. Zaidi kuhusu nodi.
  • Waandishi wa EIP: watu hawa hupendekeza mabadiliko kwenye itifaki ya Ethereum, kwa njia ya Mapendekezo ya Uboreshaji wa Ethereum (EIPs). Zaidi kuhusu EIPs.
  • Wathibitishaji: watu hawa huendesha nodi zinazoweza kuongeza vizuizi vipya kwenye blockchain ya Ethereum.
  • Wasanidi wa Itifaki (a.k.a. "Wasanidi wa Msingi" ): watu hawa hudumisha utekelezaji mbalimbali wa Ethereum (k.m., go-ethereum, Nethermind, Besu, Erigon, Reth kwenye safu ya utekelezaji au Prysm, Lighthouse, Nimbus, Teku, Lodestar, Grandine kwenye safu ya makubaliano). Zaidi kuhusu wateja wa Ethereum.

Kumbuka: mtu yeyote anaweza kuwa sehemu ya makundi haya mengi (k.m., msanidi wa itifaki anaweza kutetea EIP, na kuendesha kithibitishaji cha Mnyororo Kioleza, na kutumia programu za DeFi). Hata hivyo, kwa uwazi wa dhana, ni rahisi zaidi kuwatofautisha.

Nini maana ya pendekezo la uboreshaji wa Ethereum (EIP)?

Mchakato mmoja muhimu unaotumika katika utawala wa Ethereum ni pendekezo la Mapendekezo ya Uboreshaji wa Ethereum (EIPs). Pendekezo la uendelezaji wa Ethereum ni viwango vinavyobainisha vipengele vipya vinavyoweza kuongezwa au utaratibu mpya kwa Ethereum. Mtu yeyote ndani ya jumuiya ya Ethereum anaweza kuunda pendekezo la uendelezaji wa Ethereum. Iwapo una nia ya kuandika pendekezo la uendelezaji wa Ethereum au kushiriki katika mapito ya wenzao na\au utawala, tazama:

Zaidi kuhusu EIPs

Mchakato rasmi

Utaratibu rasmi kwa kuianza mabadiliko kwenye itifaki ya Ethereum ni kama inavyoelezwa:

  1. Pendekeza EIP ya Msingi: kama ilivyoelezwa katika EIP-1opens in a new tab, hatua ya kwanza ya kupendekeza rasmi mabadiliko kwa Ethereum ni kuielezea kwa undani katika EIP ya Msingi. Hii itafanya kazi kama vipimo rasmi kwa pendekezo la utekelezaji wa Ethereum ambayo waundaji wa programu wa itifaki watatekeleza endapo itakubaliwa.

  2. Wasilisha EIP yako kwa Wasanidi wa Itifaki: pindi unapokuwa na EIP ya Msingi ambayo umekusanya maoni ya jamii, unapaswa kuiwasilisha kwa Wasanidi wa Itifaki. Unaweza kufanya hivyo kwa kuipendekeza kwa ajili ya majadiliano kwenye simu ya AllCoreDevsopens in a new tab. Kuna uwezekano kwamba baadhi ya majadiliano yatakuwa yamefanyika kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwenye jukwaa la Ethereum Magiciansopens in a new tab au kwenye Ethereum R&D Discordopens in a new tab.

Matokeo yanayoweza kutokea katika hatua hii ni:

  • Pendekezo la uendelezaji wa Ethereum itazingatiwa kwa ajili ya sasisho ya wavu ijayo.
  • Mabadiliko ya kiufundi itahitajika.
  • Inaweza kukataliwa ikiwa haliwezi kuzingatiwa kama kipaumbele au maboresho hayatoshi kulingana na jitihadi za maendeleo.
  1. Rudia kuelekea pendekezo la mwisho: baada ya kupokea maoni kutoka kwa washikadau wote husika, kuna uwezekano utahitaji kufanya mabadiliko kwenye pendekezo lako la awali ili kuboresha usalama wake au kukidhi mahitaji ya watumiaji mbalimbali vyema. Mara tu pendekezo la uendelezaji wa Ethereum imejumuisha mabadiliko yote unayooyadhania ni muhimu, utahitaji kuwasilisha tena kwa watengenezaji wa itifaki. Kisha utaendelea kwenye hatua inayofuata ya utaratibu huu, au matatizo mapya yatatokea, yanayohitaji kurekebisha pendekezo lako tena.

  2. EIP Imejumuishwa katika Uboreshaji wa Mtandao: ikichukuliwa kuwa EIP imeidhinishwa, imejaribiwa na kutekelezwa, hupangwa kama sehemu ya uboreshaji wa mtandao. Kutokana na gharama kubwa za kuratibu maboresho ya wavu (kila mmoja anahitaji kusasisha kwa wakati mmoja), Pendekezo la uendelezaji wa Ethereum kwa kawaida huunganishwa pamoja katika maboresho.

  3. Uboreshaji wa Mtandao Umewashwa: baada ya uboreshaji wa mtandao kuwashwa, EIP itakuwa hewani kwenye mtandao wa Ethereum. Kumbuka: maboresho ya mtandao kwa kawaida huwashwa kwenye testnets kabla ya kuwashwa kwenye Mainnet ya Ethereum.

Mtiririko huu, ingawa umefanywa kwa urahisi sana, unatoa muhtasari wa hatua muhimu za mabadiliko ya itifaki yanapopelekwa kwenye Ethereum. Sasa, tazama sababu zisizo rasmi zinachangia katika utaratibu huu.

Mchakato usio rasmi

Kuelewa kazi ya awali

Washirika wanaoongoza pendekela la uendelezaji wa Ethereum wanapaswa kujifahamisha na kazi na mapendekezo za awali kabla ya kuunda pendekezo ya uendelezazi wa Ethereum ambayo inaweza kuzingatiwa kwa umakini ili kutekelezwa kwenye wavu kuu la Ethereum. Kwa njia hii, pendekezo la uendelezaji wa Ethereum inatarajiewa kuleta kitu kipya ambapo hakijakataliwa hapo awali. Sehemu kuu tatu za kufanyia utafiti huu ni hazina ya EIPopens in a new tab, Ethereum Magiciansopens in a new tab na ethresear.chopens in a new tab.

Vikundi vya kazi

Rasimu ya awali ya pendekezo ya uendelezaji wa Ethereum haiwezi kutekelezwa kwenye wavu kuu la Ethereum bila marekebisho au mabadiliko. Kwa ujumla, vinara wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum watafanya kazi na sehemu ndogo ya watengenezaji wa itifaki ili kubainisha, kutekeleza, kujaribu, kurudia na kukamilisha pendekezo lao. Kihistoria, vikundi hivi vya kazi vimehitaji miezi kadhaa (na wakati mwingine miaka!) ya kazi. Vivyo hivyo, vinara wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum kwa mabadiliko kama haya wanapaswa kuwahusisha watengenezaji wa maombi rasmi/tumiaji husika mapema katika juhudi zao ili kukusanya maoni kutoka kwa watumiaji wa mwisho na kupunguza hatari yoyote ya utekelezaji.

Makubaliano ya jamii

Wakati baadhi ya pendekezo za uendelezaji wa Ethereum ni maboresho rahisi ya kiufundi yasiyo na ukinzani mkubwa, mengine ni magumu zaidi na yanakuja na masharti ya kuchagua kati ya mambo fulani ambayo yataathiri washiriki wenye maslahi tofauti kwa njia tofauti. Hii inamaanisha baadhi ya pendekezo la uendelezaji wa Ethereum zenye utata zaidi ndani ya jamii kuliko zingine.

Hakuna mwongozo ulio wazi wa jinsi ya kushughulikia mapendekezo yenye utata. Hii ni matokeo ya muundo wa Ethereum usio na mamlaka ya kati ambapo hakuna kundi la washiriki wenye maslahi linaloweza kulazimisha jingine kwa nguvu za moja kwa moja: watengenezaji wa itifaki wanaweza kuamua kutozingatia mabadiliko ya msimbo; waendeshaji wa kituo wanaweza kuamua kutotumia mteja mpya wa Ethereum; na timu za maombi rasmi pamoja na watumiaji wanaweza kuamua kutoendesha miamala kwenye mnyororo. Kwa kuwa watengenezaji wa itifaki hawana njia ya kulazimisha watu kukubali uboreshaji ya wavu, kwa kawaida wataepuka kutekeleza pendekezo la uendelezaji wa Ethereum pale ambapo ubishi wake unazidi manufaa kwa jumuiya pana.

Mabingwa wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum wanatarajiwa kuomba maoni kutoka kwa washiriki wenye maslahi wote husika. Iwapo utakua bingwa wa pendekezo la uendelezaji wa Ethereum yenye utata, unapaswa kujaribu kushughulikia pingamizi ili kujenga makubaliano kuhusu pendekezo la uendelezaji wa Ethereum yako. Kwa kuzingatia ukubwa na utofauti wa jumuiya ya Ethereum, hakuna kipimo kimoja (k.m., kura ya sarafu) kinachoweza kutumika kupima makubaliano ya jamii, na Watetezi wa EIP wanatarajiwa kubadilika kulingana na mazingira ya pendekezo lao.

Zaidi ya usalama wa wavu la Ethereum, uzito mkubwa kihistoria umewekwa na watengenezaji wa miongozo ya itifaki juu ya kile ambachowatengenezaji wa maombi rasmi/vfaa na watumiaji wa maombi tasmi wanathamini, ikizingatiwa kwamba wao kutmia na kujenga juu ya Etheeum ndicho kinachoufanya mfumo ikolojia kuwa na kuvutia kwa washiriki wenye maslahi wengine. Zaidi ya hayo, pendekezo la uendelezaji wa Ethereum zinahitaji kutekelezwa katika utekelezaji wote wa wateja, ambao inasimamiwa na timu tofauti. Sehemu ya utaratibu huu kwa kawaida inamaanisha kushawishi timu nyingi za watengenezaji itifaki kwamba mabadiliko fulani yana thamani na kwamba inawasaidia watumiaji wa mwisho au kutatua tatizo la usalama.

Kushughulikia kutokubaliana

Kuwa na washiriki wenye maslahi wengi wenye msukumo na imani tofauti ina maana kuwa kutokubaliana si jambo nadra.

Kawaida, kutokubaliana kunashughulikiwa kupitia mijadala mirefu kwenye majukwaa ya umma ili kuelewa chanzo cha tatizo na kuruhusu mtu yeyote kutoa maoni yake. Kawaida, kundi moja hukubali kusalimu amri, au suluhu ya kati hupatikana. Ikiwa kundi moja litahisi kwa nguvu ya kutosha na kulazimisha mabadiliko fulani, inaweza kusababisha mgawanyiko wa mnyororo. Mgawanyiko wa mnyororo hutokea pale washiriki wenye maslahi fulani wanapopinga utekelezi wa mabadiliko ya kanuni za mtandao, na kusababisha matoleo tofauti yasiyooana na itifaki kuendeshwa, ambapo mnyororo miwili tofauti ya minyororo wa vizuizi hutokea.

Uma wa DAO

Mgawanyiko ni pale ambapo masasisho makubwa ya kiteknolojia au mabadiliko yanahitajika kufanywa kwenye mtandao na kubadilisha kanuni za itifaki. Ethereum clients lazima wasasishe programu zao ili kutekeleza sheria mpya za uma.

Uma wa DAO ulikuwa ni jawabu kwa shambulio la DAO la 2016opens in a new tab ambapo mkataba usio salama wa uliibiwa zaidi ya ETH milioni 3.6 katika udukuzi. Mgawanyiko huo ulihamish fedah kutoka kwenye mkataba wenye hitilafu hadi mkataba mpya, na hivyo kuruhusu yeyote aliyepoteza fedha katika udukuzi kuzirudisha.

Njia hii ya utekelezaji iliamuliwa kwa kura na jamii ya Ethereum. Mmiliki yeyote wa ETH aliweza kupiga kura kupitia muamala kwenye jukwaa la kupigia kuraopens in a new tab. Uamuzi wa kugawanya ilifika zaidi ya asilimia 85 ya kura.

Ni muhimu kutambua kwamba ingawa itifaki iligawanyika ili kurekebisha udukuzi, uzito wa kura katika kufanya uamuzi wa kugawanyika lenye utata kwa sababu kadhaa.:

  • Idadi ya wapiga kura walishiriki walikua kidogo mno.
  • Watu wengi hawakujua kuwa kura ilikua ikiendelea.
  • Kura hiyo iliwakilisha tu wamiliki wa ETH, si washiriki wengine wowote katika mfumo huo.

Sehemu ya jamii ilikataa kufanya mgawanyiko wa itifaki, hasa kwa sababu walidhani tukio ya DAO halikua hitilafu katika itifaki. Waliendelea na kuunda Ethereum Classicopens in a new tab.

Leo, jamii ya Ethereum imekubali kanuni ya kutokuingilia kati katika hali za hitilafu za mikataba au fedha zilizopotea ili kudumisha usawa unaoaminika wa mfumo.

Tazama zaidi kuhusu udukuzi wa DAO.:

Manufaa ya kuunda uma

Mgawanyo wa Ethereum / Ethereum asili ni mfano mzuri wa mgawanyiko wa itifaki yenye afya. Tulikua na vikundi viwili vilivyotofautisha sana kuhusu baadhi ya thamani za msingi, kiasi cha kuhisi kuwa hatari iliyoambatana na kufuata njia zao maalum za utekelezaji ilikua inafaa.

Uwezo wa kufanya mgawanyiko wa itifaki mbele ya tofauti kubwa za kisiasa, kifikra au kiuchumi una mchango mkubwa katika mafanikio ya usimamizi wa Ethereum. Bila uwezo wa mgawanyiko wa itifaki, mbadala ingekuwa ni migongano ya ndani inayoendelea, ushiriki usio wa hiari kwa wale ambao hatimaye waliunda Ethereum asili na maono yanayobadilika kila wakati kuhusu jinsi mafanikio ya Ethereum yanavyopaswa kuonekana.

Utawala wa Mnyororo Kioleza

Utaratibu wa usimamizi wa Ethereum mara nyingi unabadili kasi na ufanisi kwa ajili ya uwazi na ujumuishaji. Ili kuhakikisha maendeleo ya mnyororo wa taa ya mwongozo, ilianzishwa tofauti na wavu wa Ethereum wa uthibitisho wa kazi na kufuata taratibu zake za usimamizi.

Ingawa ufafanuzi na utekelezaji wa maendeleo daima imekua chanzo wazi kikamilifu, utaratibu rasmi wa kupendekeza maboresho iliyoelezwa hapo juu haukutumiwa. Hii iliwezesha mabadiliko kutambulia na kukubalika haraka ziaidi na watafiti pamoja na wale wanaotekeleza maboresho.

Wakati Mnyororo Kioleza ulipounganishwa na safu ya utekelezaji ya Ethereum mnamo Septemba 15, 2022, Muungano ulikamilika kama sehemu ya uboreshaji wa mtandao wa Paris. Pendekezo la EIP-3675opens in a new tab lilibadilishwa kutoka 'Wito wa Mwisho' hadi 'Mwisho', na kukamilisha mpito hadi uthibitisho wa hisa.

Zaidi kuhusu Muungano

Ninaweza kushiriki vipi?

Masomo zaidi

Usimamizi wa Ethereum haiko wazi kwa utaratibu thabiti. Washirika mbalimbali wa jamii wana mitazamo tofauti kuhusu hilo. Hapa kuna baadhi yao.:

Ukurasa ulihaririwa mwisho: 15 Februari 2026

Je! makala haya yamekusaidia?